Numbers 10:17-21

17 aNdipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

18 bVikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao. 19Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni, 20 cnaye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi. 21 dKisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

Copyright information for SwhKC